|
Eneo la mafinji Barabara ya lupiro -Malinyi Wilaya ya Ulanga (Ulanga Magharibi) |
|
|
Uhalibifu wa miundo mbinu katika msimu wa mvua katika wilaya ya ulanga na Kilombero limekuwa ni jambo la kawaida ambapo wananchi ndio wamekuwa wakiangaika kwa usafiri na ikiwa ni pamoja na usafirishaji wa mazao, wagonjwa na mambo mengine.
|
Huu si Mto ni barabara Mafinji Msitu nambiga |
Mvua za mwaka huu zimeleta maafa makubwa zaidi katika maeneo mbalimbali katika wilaya ya Ulanga na Kilombero ambapo katika eneo la Mafinji msitu wa Nambiga hali imekuwa mbaya zaidi, licha ya kukatika kwa daraja katika eneo hilo ambapo wananchi walikaa kwa muda wa zaidi ya wiki bila kuwepo usafiri wa kuvuka eneo hilo,mara baada ya kutengenezwa kwa daraja hilo hali ya kuharibika kwa barabara eneo hilo ikajitokeza hadi sasa hakuna matengenezo yeyote yaliyofanyika yapata zaidi ya mwezi mmoja.
|
Eneo la mafinji (ulanga magharibi) |
|
|
Wakatia hayo yakiendelea Ulanga magharibi, Ulanga mashariki barabara nayoimekuwa tatizo eneo la fimbo limekuwa likiharibika kila mwaka na mwaka huu imekuwa balaa zaidi.
|
Eneo la fimbo, Ulanga Mashariki |
kwa mujibu wa mkaguzi wa kifusi kutoka Daino Tec Mohamed Juma watengenezaji wa barabara wilayani hapa wamesema kilicho fanyika kwa sasa ni kuweka mawe katika mashimo hayo na matengenezo yatategemea kukatika kwa mvua,huku akimlalamikia mkandarasi wa barabara ya Malinyi kutokomea kusiko julikana bara baada ya kulipwa fedha za awali za kazi aliyokwisha fanya.
|
maeneo ya Ilagua Ulanga njia ya Malinyi |
Tayari Mkuu wa mkoa wa Morogoro amefika kutemberea maeneo ya mafuriko katika mto kilombero ambapo hadi sasa huduma ya kivuko imesimamishwa kwa muda usio julikana kutokana na kivuko hicho kushindwa kustahimili nguvu ya maji.
|
MV KILOMBERO II |
Hadi jana mvua zimeendelea kunyesha wilayani ulanga na kilombero hali inayozidi kuleta hofu kwa rai, wakati huo huo huko mbingu Mngeta kunariportiwa kuwepo kwa mafuriko.
je hali hii ya miundo mbinu nani alaumiwe?
No comments:
Post a Comment