- Maji yaendelea kuongezeka
- Usafiri bei juu
Mkuu wa wilaya ya Ulanga akiwa katika moja ya moti kivukoni siku ya mei mosi katika ziara. ya kukagua hali ya huduma kivukoni. |
Wito umetolewa kwa wamiliki
wa boat ndogo katika maeneo mbali mbali kuzileta katika mto kilombero ilikutoa
huduma ya usafiri kwa wakazi wa Kilombero na Ulanga kutokana na maji kuendelea
kuongezeka katika mto Kilombero.
Hayo yamesemwa na mkuu wa
wilaya ya Ulanga MH, Francesi Miti
wakati akizungumza na wananchi wa
kivukoni na wasafiri jana katika eneo la kivuko alipofika kuangalia hali ya
huduma za usafiri katika mto Kilombero.
Mitti amewataka wasafiri wote wanaotumia usafiri wa boat zilizopo
sasa ambazo ni boti ya sakosi, boti ya halmashauri ya wilaya ya ulanga, boat ya
sua, kuvaa maboya ilikuweza kuwa salama zaidi wanapo kuwa katika vyombo hivyo
vya usafiri.
Mapema Miti akiwa katika eneo
hilo wananchi
na wasafiri walilalamikia bei ya boat hizo ambapo mtu mmoja alikuwa akivushwa
kwa shilingi 2000 kutoka bei ya kawaida ya shilingi 200 kwa pantoni ya kivuko,ambapo baada ya
mazungumzo na wasafirishaji bei imeshuka hadi kufikia shilingi 1500 kwa mtu
mmoja, huku mitumbwi ikipigwa marufuku kutoa huduma ya usafiri kutokana na kasi
ya maji katika mto kilombero.
Miti aliambatana na kamati ya
Ulinzi na usalama wilaya, kaimu mkurugenzi wa wilaya ya ulanga, mwenyekiti wa
chama cha ccm wilaya ya ulanga, viongozi mbalimbali wa serikali na wajumbe
wengine wa chama.
No comments:
Post a Comment