- Wachina wapagawa, wafanya kazi usiku na mchana
- Makalavati ya hitajika
- Miundo mbinu ya daraja la kilombero/Ulanga kubadirishwa.
Hali ya barabara kati ya
ulanga na kilombero katika eneo la kivukoni upande wa ifakara imeendelea kuwa
mbaya kutokana na wakandarasi kushindwa kudhibiti maji yanayo bomoa barabara
hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo ya
Mkandarasi mshauri bwana Saidi Atikhula amesema maji yameongezeka kwa kiasi
kikubwa mno na yamekuwa na kasi kubwa hali inayofanya shuhuli nzima ya kuweka
mawe ili kuziba maeneo yaliyobomoka kuwa ngumu.
katapila likiendelea na kazi |
Bwana Atikhula amesema hadi
jana wamesha mwaga zaidi ya tripu136 za mawe katia maeneo yaliyo katika
barabara lakini maji yamekuwa na nguvu na kubomoa barabara sehemu nyingine,
ambapo hadi hivi sasa barabara imekatika mara 3 huku maeneo mengine yakiendelea
kubomoka.
Aidha amesema kuwa, shughuli ya uwekaji mawe haifai
kutatua tatizo hilo, isipokuwa nikutafuta makaravati na kuweka katika maeneo
ambayo barabara imekatika, na itahitaji kusubiri maji yapunguwe na kwamba kwa
sasa wao hawana vifaa hivyo na wameshindwa kuendelea na uzibaji wa maeneo hayo.
Mkandarasi mshauri SAIDI ATIKHULA wapili kutoka kulia akitoa ufafanuzi kwa mkuu wa wilaya ya Ulanga Francis Mitti |
Atikhula akizungumza mbele ya
mkuu wa wilaya ya ulanga, Francis Mitti amesema maji yamejaa zaidi ya kipimo
cha mwisho cha ujazo wa maji katika mto
Kilombero na kuna hatari ya barabara nzima kusombwa na maji katika eneo
hilo la kivukoni.
Eneo linalo jazwa mawe |
Nini kilicho amuliwa?
Mkandarasi amemweleza kwa
njia ya simu meneja wa barabara Mkoa juu ya tatizo zima na imeamuliwa yatafutwe
makalavati kutoka maeneo mbalimbali ilikuja kutatua tatizo hilo.
Wakati huo huo hali ya
usafiri katika eneo hilo imeendelea kuwa ngumu baada ya maji kuongezeka
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo umbali wa kusafiri kwa boti
umekuwa nimkubwa zaidi.
Abilia wakipanda boat |
Mapema nauli ya boti ilikuwa
ni shilingi 2000 kwa mtu mmoja kabla ya mkuu wa wilaya ya ulanga kushauliana na
waendesha boti hizo baada ya kusikia malalamiko ya wananchi na wasafiri katika
eneo hilo la kivukoni na kufikia
shilingi 1500 huku mitumbwi ikipigwa marufuku kutoa huduma.
kivuko kikiwa kimepaki kivukoni |
Matumaini ya kivuko kilicho simamishwa kuvusha watu na mali zao kurejea kufanya kazi ni madogo kutokana na maji hayo kuongezeka ambapo hadi jana maji yalikuwa yameongezeka ujazo wa mita 9 kutoka ujazo wa kawaida wakuweza kivuko hicho kufanya kazi. kivuko kinahitaji maji yapunguwe kwa ujazo wa mita 3 hadi nne ili kiweze kufanya kazi angalau kwa kubeba watu wachache na magarin na mizigo.
Hali ya bidhaa Mahenge ulanga ikoje?
Hali ya bidhaa mbalimbali katika
wilaya ya ulanga
imeanza kupanda ambapo mafuta ya petroli katika mji wa Mwaya ni shilingi 3000
kwa lita huku Lupiro ikiwa ni shilingi 2500, vileo katika mji wa mahenge katika
baadhi ya baa bia zimefikia shilingi 2500 kwa chupa huku chipsi kavu zikiuzwa
1500 chipsi mayai 2500.
Bidhaa zikiwa ndani ya mtumbwi |
Hali ya kupanda bidhaa
inawezekana ikaendelea kutokana
na kuwepo kwa ugumu wa uvushaji katika mto kilombero ambapo wafanya
biashara wamekuwa wakitozwa bei kubwa ya usafirishaji.
UJENZI WA DARAJA HALI IKOJE?
Kwa mujibu wa Said Atikhula ambaye ndie msimamizi na mshauri wa mradi wa daraja la mto kilombero amesema kunahaja ya kubadili eneo lililopangwa kujengwa daraja hilo.
Moja ya kalavati likiwa limezama kwenyemaji |
Atikhula amesema shughuli zote zimesimama hadi hapo maji yatakapo pungua kwa sababu eneo lote limezungukwa na maji.
UKWELI NI UPI JUU YA MCHINA ALIYE JINYONGA?
Kwa mujibu wa Said Atikhula mchina aliyejinyonga hausiani na shughuli ya ujenzi wa daraja na alikuwepo ifakara eneo la kivukoni kwa muda wa siku 15 tu na alikuwa anamatatizo yakifamilia huko kwao china naalikuja nchini kupumzika,
Ndugu na rafiki wa mchina aliyejinyonga wakitoa ufafanuzi msichana ni mkalimani wa wachina |
Amesema kijana huyo wa kichina aliyefahamika kwa jina la Qin Baofeng hana utaalamu wowo juu ya ukandarasi na hakua na mamlaka yeyote katika kazi hiyo.
Mapema taarifa zilizo zagaa zilidai mchina huyo alijiua kutokana na kuona ujenzi wadaraja umekuwa mgumu.
Mwili wa kijana huyo wakichina amesafirishwa jana kwenda dar es salaam.
ENDELEA KUFUATILIA BLOG HII PICHA ZA MATUKIO MBALI MBALI COMING SOON
No comments:
Post a Comment