Karibu Dj Dukeswagas blog

Monday, May 5, 2014

MKUU WA MKOA MOROGORO ATEMBELEA MTO KILOMBERO

  • Hali bado yaendelea kuwa tete
kivukoni
Kufuatia hali mbaya inayoendelea kujitokeza katika mto Kilombero Imemlazimu mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera kufika leo katika mji wa Ifakara eneo la kivukoni kujionea hali ilivyo.

Akiwa katika eneo la kivukoni bendera amesema kuwa kupitia ofisi yake atajitahidi kuhakikisha hali hapo kivukoni inarejea katika hali ya kawaida ndani ya siku sita kama maji yatapungua na mvua kusimama kunyesha.

amesema kuwa kutokana na hali ilivyo mamlaka ya barabara taifa nao watakuja kuangalia jinsi ya kutatua tatizo hilo,.

Mkuu wa mkoa ameambatana na Meneja tan road Mkoa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama mkoa.

Hadi sasa maji hayajapungua katika mto Kilombero na hali ya usafiri ni bado ngumu hadi sasa, kwa mujibu wa msimamizi wa Ukandarasi wa eneo hilo amesema hali ya kurejesha barabara katika hali ya kawaida itategemea kupatikana kwa makaravati na kupungua kwa maji, ambapo kama itakuwa hivyo ujenzi utachukua siku 6.

Ni mafuriko makubwa kutokea katika Mto kilombero ukilinganisha na mafuriko ya mwaka 1979.



1 comment: