Mashindano ya miss kilombero
yamefanyika jumamosi iliyopita
katika ukumbi wa jamosi mjini ifakara ambapo washiriki zaidi ya 13 walipanda
jukwaani katika kinyanganyiro hicho.
Akizungumza kabla ya kumtaja mshindi siku hiyo mratibu wa
miss Tanzania mkoa wa morogoro Frank
Kikambako alisema mashindano hayo yamezingatia vigezo vyote hadi kufikia
kumpata mshindi wa wilaya ya kirombelo
Prisca mengi ndie aliyeibuka kidedea
katika mashindano hayo ambapo alijinyakulia kitita cha shilingi laki 300,000 na
huku akipokea kiasi cha shilingi 120,000 kwa kushinda kipengere cha talelent
wakati huo huo akipokea kioo chenye thamani ya shilingi 150,000 kutoka kwenye
kampuni ya Tonialuminiamu ya mjini ifakara. Hapa anaeleza furaha yake
Miss Kilombero 2012 Prisca Mengi. |
Mshiri kutoka mlimba Modesta Wella
ndiye aliyeibuka katika nafasi ya pili akijinyakulia kitita cha shilingi
250,000 na kioo chenye thanmani ya shilingi 150,000 kutoka toni aluminiamu
akifuatiwa na Nafia Waziri kutoka mang’ura aliyeshinda nafasi ya tatu.
Baadhi ya watu walioshiriki mashindano hayo wamewapongeza
waratibu wa mashindano hayo kwa kusema mashindano yalikuwa mazuri na watu
walipata nafasi nzuri ya kuwaona washiriki bila msongamano.
Washiriki wakiwa katika jukwaa kabla ya kutajwa kwatano bora |
AIDHA Bwana ngailo amesema kwa sasa
wanajipanga katika kuwaandalia washiriki watano
wa lioingia katika tano bora mazingira mazuri ya kushiriki miss mkoa
ambayo ratiba yake bado haijatolewa amewaomba washiriki hao kuendelea kujipanga
vizuri kwa mashindano hayo.
Mashindano ya miss kilombero kuelekea miss Tanzania
yanafanyika kwa mara ya tatu sasa toka yaanzishwe mwaka 2010 ambapo yamekuwa
yakisimamiwa na jamosi Entertaiment.
Kama unamaoni ingia kwenye box ya coment hapo chini.
kaka haujafanya shift humu kweliiii!!!!!!!!!!!!!
ReplyDelete