Karibu Dj Dukeswagas blog

Wednesday, May 9, 2012

HALI YA BARABARA IFAKARA - MAHENGE YAZIDI KUWA TETE



 MABASI YA LALANJIANI
  • Watembea kwa miguu watereza, wapanda baiskeli hadi pikipiki.
 Barabara ya kutoka Ifakara kwenda Mahenge wilayani Ulanga imezidi kuwa mbaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo. Baadhi ya wasafirishaji wa abiria na mizigo wamemlalamikia mkandarasi ambaye ametengeneza barabara hiyo kwa msimu huu kwa kitendo cha kupitisha katapila na kukwangua udongo uliojishindilia na kuuacha bila kuushindilia hali iliyopelekea magari kuanza kukwama baada ya mvua kunyesha.

Moja ya basi linalofanya safari kati ya Mahenge na Dar  es Salamu kampuni ya Moro best  likiwa Limekwama Eneo la Nalukoo.

Hivi karibuni zaidi ya magari 10 yalilazimika kulala katika eneo hilo baada ya roli kuziba njia, usishangae kwa vyombo vya usafiri kutoka pande hizi ukikuta wamebeba pumba za mpunga au michanga nafaka hiyo hutumika kuweka maeneo mabichi ilikusaidia kuweka ukavu.

Hii ndio halialisi ilivyo Eneo la nalukoo Ulanga


Wasafiri wakitembea kwa miguu baada ya kushuka kutoka katika basi la alsaidi ilikupisha gari hilo liweze kupita,mithiri ya kwenda kwenyekikombe kwa babu loliondoooo.





Msimu huu bara bara nyingi za wilaya ya kilombero na ulanga hua katika hali mbaya kutokana na haliya aridhi hiyo kuwa na tabia ya kutunza maji na utengenezaji wa barabara usiozingatia vigezo kama kuweka tope badala ya changalawe au kokoto.

No comments:

Post a Comment