Waziri wa ofisi ya raisi menejimenti ya utumishi wa umma mh
Celina Kombani ambaye pia ni mbunge wa
ulanga mashariki anatarajia kufanya ziara ya siku 2 katika jimbo la wilaya ya ulanga kuanzia may 11 mwaka huu
Katika ziara hiyo waziri kombani atatembelea tarafa za vigoi
na mwaya ambapo atakabidhi miradi ya visima vya maji kwenye shule za sekondari
na msingi
Aidha imebainishwa kuwa, tarehe kumi na moja Kombani atakuwa
tarafa ya mwaya na tarehe kumi na mbili atakuwa tarafa ya vigoi
Hata hivyo wananchi wote mnatakiwa kuhudhuria katika ziara
hiyo ili kuweza kuleta ushirikiano kwa mheshimiwa Kombani
No comments:
Post a Comment