Karibu Dj Dukeswagas blog

Friday, May 11, 2012

THE BEAT POWER INFO. COM


The beat power infor .com
 

Sam wa ukweli na ngoma yake mpya inayojulikana kwa jina la najua ngoma hiyo nayo ni ya kimalavidave kikubwa kinacho jitokeza katika ngoma hiyo ni jinsi anavyo pangilia maneno na misemo.
 Katika rekodi hiyo kuna maneno kama, nilikukabidhi kitanda changu chenye shuka thamani, nimekula samaki mtamu kama nini lakini mwiba umenichoma je samu nikweli yamemtokea au laaa. Usikose exclusive interview na mzichi.  Songi linapatikana kupitia (91.2 Ulanga Fm



Wazee wa kazi kutoka ulanga fm good laki mshahiri na Godwin mawanja wameachia kazi yao ya kwanza katika muundo wa soft crank inayoitwa unavyo dresi.
Wakizungumza na kurasa ya ifo .com ya the beat power wamesema ngoma hiyo wametoa kama burudani ya kawaida tu kwa wasikilizaji na hawakuipangilia kivile licha ya mashabiki kuikubali toka walipoitambulisha katika the beat power hivi karibuni.
Mshairi aka gm one ambaye ndie producer wa ngoma hiyo amesema bado wanajipanga kwa kuachia ngoma za ukweli sasa ambazo hizo zitakuwa rasmi.
Wamesema katika kuwafurahisha mashabiki watapanda jukwaani siku ya ladies free kuonyesha maujanja binafsi siku ya leo ijumaa katika kuitambulisha ngoma hiyo.


MSANII LINEX WENGI WANAPENDA KUMWITA  "MJEDA" AMEACHIA NGOMA YAKE MPYA INAYOKWENDA KWA JINA LA "AIFORA', IKIWA NI SINGLE YAKE YA 3 KUACHIA MWAKA HUU TANGU UANZE,
NGOMA YAKE YA KWANZA KUACHIA ILIKUWA "MACHO YANGU JUU" AMBAYA ILIKUWA YA KUNDI ZIMA.  BAADA YA HII AMEACHIA SINGLE NYINGINE INAITWA "NITAIFICHA WAPI" SINGLE AMBAYO AMEMSHIRIKISHA MSANII DIAMOND AMBAYO INAFANYA VIZURI SASAHIVI KWENYE VITUO MBALIMBALI VYA REDIO,
LINEX AMEACHIA MZINGO MWINGINE MATATA SANA.....HAKIKA WIMBO HUU UKIHUSIKIA UTAKUKUNA SANA....WIMBO AMBAO UTAKUJA KUFANYA VIZURI SANA WIMBO HUU MPYA AMBAO UNAITWA "AIFORA" UMESIMAMIWA NA PRODUCER ANAYEITWA  "FUNDI SAMWELI". HAYA KAZI KWENU WASIKILIZAJI NA MASHABIKI WA "MJEDA LINEX" NA MKAE MKAO WA KUSUBIRI VIDEO YAKE YA WIMBO HUU AIFORA..!
AKIZUNGUMZIA JUU YA NGOMA HIYO MJEDA AMESEMA NGOMA HIYO INASTORY YA KWELI NDANI YAKE AMBAPO ANAJARIBU KUONESHA KUWA NI WATU WENGI AMBAO HUWATHAMINI NA KUWAPENDA WAPENZI WAO LAKINI  WAPENZI HOA HUWA NIWALAGHAI TU.

Wednesday, May 9, 2012

MAJINA MAPYA YA WAKUU WA WILAYA YATANGAZWA


WAZIRI MKUU ATANGAZA MAJINA YA WAKUU WA WILAYA WAPYA 70 NA
VITUO VYAO VYA KAZI
Siku chache baada ya kutangazwa kwa baraza jipya la mawaziri, waziri mkuu Mizengo Pinda leo hii ametangaza majina mapya ya wakuu wa wilaya na vituo vyao vya kazi,wakiwemo waandishi na watangazaji wa habari kama Novatusi Makunga kutoka ITV aliyekuwa ripoter,
Pinda amesema uteuzi huo umezingatia vigezo stahiki kwa kuangali uhitaji, usawa kati ya wanaume na wanawake. wilaya ya Ulanga imebakiwa na Mkuu yule yule wa awali MH Francisi Miti, huku kirombero akiwa ni Hassani E. Masala ambaye ameziba pengo la wilaya hiyo kutokuwa na mkuu wa wilaya kwa muda mrefu.
1. Novatus Makunga Hai
2. Mboni M. Mgaza Mkinga
3. Hanifa M. Selungu Sikonge
4. Christine S. Mndeme Hanang
5. Shaibu I. Ndemanga Mwanga
6. Chrispin T. Meela Rungwe
7. Dr. Nasoro Ali Hamidi Lindi
8. Farida S. Mgomi Masasi
9. Jeremba D. Munasa Arumeru
10. Majid Hemed Mwanga Lushoto
11 Mrisho Gambo Korogwe
12. Elias C. J. Tarimo Kilosa
13. Alfred E. Msovella Kiteto
14. Dkt. Leticia M. Warioba Iringa
15. Dkt. Michael Yunia Kadeghe Mbozi
16. Mrs. Karen Yunus Sengerema
17. Hassan E. Masala Kilombero
18. Bituni A. Msangi Nzega
19. Ephraem Mfingi Mmbaga Liwale
20. Antony J. Mtaka Mvomero
21. Herman Clement Kapufi Same
22. Magareth Esther Malenga Kyela
23. Chande Bakari Nalicho Tunduru
24. Fatuma H. Toufiq Manyoni
25. Seleman Liwowa Kilindi
26. Josephine R. Matiro Makete
27. Gerald J. Guninita Kilolo
28. Senyi S. Ngaga Mbinga
29. Mary Tesha Ukerewe
30. Rodrick Mpogolo Chato
31. Christopher Magala Newala
32. Paza T. Mwamlima Mpanda
33. Richard Mbeho Biharamulo
34. Jacqueline Liana Magu
35. Joshua Mirumbe Bunda
36. Constantine J. Kanyasu Ngara
37. Yahya E. Nawanda Iramba
38. Ulega H. Abadallah Kilwa
39. Paul Mzindakaya Busega (mpya)
40. Festo Kiswaga Nanyumbu
41. Wilman Kapenjama Ndile Mtwara
42. Joseph Joseph Mkirikiti Songea
43. Ponsiano Nyami Tandahimba
44. Elibariki Immanuel Kingu Kisarawe
45. Suleiman O. Kumchaya Tabora
46. Dkt. Charles O. F. Mlingwa Siha
47. Manju Msambya Ikungi (mpya)
48. Omar S. Kwaangw’ Kondoa
49. Venance M. Mwamoto Kibondo
50. Benson Mpesya Kahama
51. Daudi Felix Ntibenda Karatu
52. Ramadhani A. Maneno Kigoma
53. Sauda S. Mtondoo Rufiji
54. Gulamhusein Kifu Mbarali
55. Esterina Kilasi Wanging’ombe (mpya)
56. Subira Mgalu Muheza
57. Martha Umbula Kongwa
58. Rosemary Kirigini Meatu
59. Agness Hokororo Ruangwa
60. Regina Chonjo Nachingwea
61. Ahmed R. Kipozi Bagamoyo
62. Wilson Elisha Nkhambaku Kishapu
63. Amani K. Mwenegoha Bukombe
64. Hafsa M. Mtasiwa Pangani
65. Rosemary Staki Senyamule Ileje
66. Selemani Mzee Selemani Kwimba
67. Lt. Col. Ngemela E. Lubinga Mlele (mpya)
68. Iddi Kimanta Nkasi
69. Muhingo Rweyemamu Handeni
70. Lucy Mayenga Uyui

MAJINA 63 WAKUU WA WILAYA WA ZAMANI NA
VITUO VYAO VYA KAZI

NA. JINA KITUO CHA KAZI
1. James K. O. Millya Longido
2. Mathew S. Sedoyeka Sumbawanga
3. Fatuma L. Kimario Igunga
4. Capt. (Mst.) James C. Yamungu Serengeti
5. Lt. (Mst.) Abdallah A. Kihato Maswa
6. Sarah Dumba Njombe
7. Jowika W. Kasunga Monduli
8. Elizabeth C. Mkwasa Bahi
9. Col. Issa E. Njiku Misenyi
10. John B. Henjewele Tarime
11. Elias W. Lali Ngorongoro
12. Raymond H. Mushi Ilala
13. Francis Miti ..Ulanga
14. Evarista N. Kalalu Mufindi
15. Mariam S. Lugaila Misungwi
16. Anna J. Magowa Urambo
17. Anatory K. Choya Mbulu
18. Fatma Salum Ally Chamwino
19. Deodatus L. Kinawiro Chunya
20. Ibrahim W. Marwa Nyang’hwale (mpya)
21. Dkt. Norman A. Sigalla Mbeya
22. Moshi M. Chang’a Mkalama (mpya)
23. Jordan M. Rugimbana Kinondoni
24. Georgina E. Bundala Itilima (mpya)
25. Halima M. Kihemba Kibaha
26. Manzie O. Mangochie Geita
27. Abdula S. Lutavi Namtumbo
28. Zipporah L. Pangani Bukoba
29. Dkt. Ibrahim H. Msengi Moshi
30. Col. Cosmas Kayombo Kakonko (mpya)
31. Lembris M. Kipuyo Muleba
32. Elinasi A. Pallangyo Rombo
33. Queen M. Mlozi Singida
34. Juma S. Madaha Ludewa
35. Angelina Mabula Butiama (mpya)
36. Hadija H. Nyembo Uvinza (mpya)
37. Ernest N. Kahindi Nyasa (mpya)
38. Peter T. Kiroya Simanjiro
39. John V. K. Mongella Arusha
40. Baraka M. Konisaga Nyamagana
41. Husna Mwilima Mbogwe (mpya)
42. Sophia E. Mjema Temeke
43. Francis Isaac Chemba (mpya)
44. Abihudi M. Saideya Momba (mpya)
45. Khalid J. Mandia Babati
46. Anna Rose Nyamubi Shinyanga
47. Dani B. Makanga Kasulu
48. Amina J. Masenza Ilemela
49. Mercy E. Silla Mkuranga
50. Christopher R. Kangoye Mpwapwa
51. Lt. Edward O. Lenga Kalambo (mpya)
52. Halima O. Dendego Tanga
53. Lephy B. Gembe Dodoma
54. Saidi A. Amanzi Morogoro
55. Jackson W. Msome Musoma
56. Elias C. B. Goroi Rorya
57. Lt. Col. Benedict Kitenga Kyerwa (mpya)
58. Erasto Sima Bariadi
59. Nurdin H. Babu Mafia
60. Khanifa M. Karamagi Gairo (mpya)
61. Gishuli M. Charles Buhigwe (mpya)
62. Saveli M. Maketta Kaliua (mpya)
63. Darry Rwegasira Karagwe

CELINA KOMBANI KUFANYA ZIARA ULANGA




Waziri wa ofisi ya raisi menejimenti ya utumishi wa umma mh Celina Kombani  ambaye pia ni mbunge wa ulanga mashariki anatarajia kufanya ziara ya siku 2 katika jimbo la  wilaya ya ulanga  kuanzia may 11 mwaka huu

Katika ziara hiyo waziri kombani atatembelea tarafa za vigoi na mwaya ambapo atakabidhi miradi ya visima vya maji kwenye shule za sekondari na msingi

Aidha imebainishwa kuwa, tarehe kumi na moja Kombani atakuwa tarafa ya mwaya na tarehe kumi na mbili atakuwa tarafa ya vigoi

Hata hivyo wananchi wote mnatakiwa kuhudhuria katika ziara hiyo ili kuweza kuleta ushirikiano kwa mheshimiwa Kombani

 

WATOTO MAPACHA WAFARIKI DUNIA KWA MOTO KATIKA KIBANDA CHA NYASI - MNGETA


MOROGORO

Watoto mapacha wenye umri wa mwaka mmoja na miezi 8 wamefariki katika ajali ya moto ndani ya  kibanda cha nyasi walimokuwa wakichezea
Kamanda wa Polisi  mkoani morogo   Adolfina Chialo amesema ajali hiyo ya moto ilitokea   katika eneo la Lukanga Mngeta wilayani Kilombero mkoani morogoro
Kamanda Chialo amesema mapacha hao waliingia katika kibanda hicho kwa lengo la kucheza, lakini baada ya muda, kibanda hicho kiliwaka moto huku mapacha hao wakiwa ndani na kusababisha kifo chao papo hapo.
Hata hivyo , Kamanda Chialo amesema kuwa uchunguzi umeanza kufanyika ili kujua  chanzo cha  moto huo.