MSANII KUTOKA MAHENGE ULANGA MOROGORO,ADAIWA KUIBA WIMBO.
Msanii mchanga wa musiki wa kizazi kipya alimaarufu kama bongo fleva Yang Simple ambaye ametamba na wimbo wake wa muda bado, hivi karibuni amedaiwa kukopi wimbo huo kutoka kwa msanii mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Tomas.
Akizungumza na ulanga fm kwa njia ya simu, kupitia kipindi
cha joto la jumamosi kinacho rushwa kila siku ya jumamosi meneja wa kampuni ya
sweet production jijini dare s salaam Wills
amesema kuwa amepokea taarifa za msanii huyo kukopi wimbo huo ambao alidai
ni utunziwake yeye mwenyewe.
Meneja huyo amedai kuwa amesikitishwa na kitendo hicho
kwakuwa msanii tom ambaye ndiye mmiliki halali wa wimbo huo,aliujumuisha wimbo
huo katika albamu yake ambayo inatarajia kuachiwa hivi karibuni.
Kwa upande wake yang simple mapema alisema wimbo huo ni
utunzi wake isipokuwa biti hanauhakika kama haina mtu kwakuwa biti hiyo
aliikuta imeshatengenezwa.
Hata hivyo baada ya kubanwa na maswali yang simple ambaye
alifadhiriwa na mtu aliye fahamika kwa jina la Eddo, alikiri kuwa wimbo huo
aliukuta kwa produsa ambaye ni rafiki yake aliye mtaja kwa jina moja la Kona,
na kwamba walibadirisha baadhi ya maneno na kuurecord kwa gharama ya shilingi
40,000 huku producer huyo akimwambia kuwa wimbo huo ni deal na uwe siri yao.
Hali hiyo imejitokeza wakati wimbo huo ukifanya vizuri katika
vituo mbalimbali vya redio, na kuwapa mshutuko baadhi ya mashabiki wa msanii
huyo.
Akizungumza kwanjia ya simu jumatatu hii yang simple
amesemama kwa sasa anaachana kwa muda na masuala ya muziki na kujikita katika
masomo kwa kuwa yupo kidato cha nne na kumtaka radhi meneja wa kampuni ya sweet
kwa hali iliyo jitokeza na kuomba wimbo huo usipigwe tena katika vituo vya
radio.
Naye meneja wa kampuni hiyo amesema kuwa anawaomba wasanii
wachanga kuacha mara moja tabia ya kukopi nyimbo zisizo zao kwakuwa kufanya
hivyo ni kosa kisheria.
Toeni elimu ya kutosha kwa vijana wanaochipukia, kuhusu umuhimu wa kujitegemea katika kufanya kazi zao kwani naamini wanatafuta njia za kutoka ingawaje wanatumia njia zisizo sahihi.. kupitia blog yako chief naamini vijana Ulanga wataelimika na wataweza kufaamu athari za kutumia/kukopi kazi za wenzao.....
ReplyDeletehiyo ndio kazi kubwa itakayo nikabili kwa sas pwaa man keep on
Delete