Karibu Dj Dukeswagas blog

Wednesday, March 14, 2012

HATARI!!!!!MNYAMA ASIE JULIKANA AINGIA MAHENGE

Katika hali isiyo yA kawaida mnyama anaye sadikika kuwa simba, Chui au Fisi amevamia mji wa Mahenge katka eneo la Chamange na kula nguruwe wapatao wa nne kwa muda wa siku nne tangu march 12 hadi leo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa eneo la chamange wamesema hawajaweza kufahamu moja kwa moja mnyama huyo ni simba au laaa lakini amekuwa akitokea nyakati za usiku na kuuwa nguruwe na kuacha Kichwa, Utumbo na Maini pamoja na viungio vya miguu.

Mtu mmoja ambaye anadai kumuona mnyama huyo amesema kuwa mnyama huyo nimkubwa na wala si mbwa wala fisi au chui kwakuwa ingawa alikuwa gizani aliweza kumuona akiwa anarangi inayo karibia kuwa nyekundu na huwenda akawa simba.

Nilimtafuta mtalamu kutoka maliaasili iliaweze kuzungumzia sakata hilo ambapo mtalamu huyo amesema wamepata taarifa kuwepo kwa mnyama huyo ila bado hawajajua kama mnyama huyo ni simba au laa. mtaalamu huyo amewataka wananchi kuwa makini na kutaembae nyakati za usiku kwakuwa mnyama huyo hutembea nyakati za usiku, na kuwataka wananchi wote wa mahenge kukata majani na vichaka vinavyo zunguka nyumbazao ikiwa ni pamoja na kutoa tarifa mara moja endapo watamuona mnyama yeyote asiye wakufugwa .

mwaka jana wananchi wakichangani waliua vitoto vya simba vitano vilivyo dhaniwa kuwa na mama yao ingawa hakuna madhara yeyote yaliyojitokeza.



1 comment:

  1. Asante kwa taarifa chief!!so wale wazee wa chupa mwisho saa 12..du basi hatari !! Lakini sio mara ya kwanza kutokea mnyama kama huyo maeneo ya hapo Nawenge wasiliana na wazee ili wakupe historia ya tukio kama hilo aidha ni mbinu gani walizitumia kupambana na tatizo hilo ili wafanikishe kumwondoa mnyama huyo..
    DED atoe night za kutosha najua makanda wapo wakotosha kwani hili ni tatizo hususani kwa mifugo na maisha ya watu..

    ReplyDelete