Uchunguzi
liofanyika na idara ya wanyamapori wilayani Ulanga mkoani morogoro, imebaini kuwa mnyama anayekula
mifugo ni fisi na siyo simba kama ambavyo wananchi walivyokuwa wakidhani
Akifafanua afisa
wanyamapori John Fanuel Makota, amesema kuwa fisi huyo anafahamika kama kanka simba ambaye ni mkubwa tofauti na fisi wa
kawaida na ana madoa madoa
Aidha amewaomba wananchi kuimarisha mabanda yao ya nguruwe na kuzingatia kutembea watu zaidi ya mmoja nyakati za usiku na kama ikibidi watu wasitembee usiku kama haakuna ulazima.
Kwa muda wa siku 5 sasa mnyama huyo amekuwa akila nguruwe katika maeneo mbalimbali ya mji wa mahenge ambapo hadi sasa nguruwe wa 5 inasemekana kuliwa.
No comments:
Post a Comment