Ray C wa kiuno bila mfupa abadilika
Ray C, ambaye ametamba kurudi rasmi na kibao cha
“Mshum Mshum”, amesema ingawa mashabiki wake walimzoea kwa umahiri wake
katika kukata viuno, sasa watarajio vitu tofauti; muziki anaoufanya ni
ule wa kuonyesha kipaji chake cha kuimba.
Akizungumza na Mwananchi, Ray C alisema mwezi huu
anatarajia kurudi rasmi katika anga za muziki kwani ameshahakikisha kuwa
harakati zake za kupambana na dawa za kulevya kupitia mfuko wake wa Ray
C Foundation, zimesimama imara hivyo ni wakati wa kurudi ili aendelee
na kampeni yake upande wa pili.
“Ninatarajia kuachia nyimbo zangu mpya za “Kiss
Kiss” au “Mshum Mshum” mwezi huu, lakini mashabiki wangu wajue kwamba
safari hii ni kuonyesha kipaji cha kuimba, hakuna mambo ya kiuno bila
mfupa, nimebadilika kwa kiasi kikubwa sana,” alisema.
Ni kitambo toka Ray C, ambaye jina lake halisi ni
Rehema Chalamila, kuonekana kwenye muziki baada ya ukimya wa muda mrefu
uliotokana na matatizo ya utumiaji wa dawa za kulevya, ambao anakiri
ulimrudisha nyuma kimaisha.
“Natamani wasanii wengine wasiguse kabisa hii
kitu. Binafsi imenirudisha nyuma sana. Kwa sasa nimesharekodi studio za
Legendary Music Studio kwa Tudd Thomas na kwingineko,” alisema.
Ray C alizidi kufunguka kwa kudai kuwa ujio wake mpya pia utahusisha nyimbo za taarabu.
“Albamu yangu ambayo inakuja hivi karibuni ina
mchanyiko wa nyimbo mbalimbali, zikiwemo taarab na za kihindi. Nimefanya
taarab kama mbili na zook, yani nimebadilika kabisa,” alisema.
kuna kwaito, kuna bongoflava,uhindi hindi kidogo,” alisema Ray C.
Chanzo mwananchi
Chanzo mwananchi
No comments:
Post a Comment