Halmashuri ya wilaya ya ulanga mkoani morogoro wametoa shukrani kwa shirika
la utangazaji lisilo la kiserikali la UINGEREZA
BBC MEDIA ACTION kwa kuwapatia msaada wa vifaa ikiwemo lapto mbili
pamoja na maranzi kwa ajili ya kurekodia vipindi vya Radio ulanga kwa ubora.
Hayo yamebainishwa hii leo na kaimu mkurugenzi wa halmashauri bwana
Benedict Mabula kwenye ukumbi wa paulin katika siku ya Radio Open Day.
Hata hivyo bwana Mabula ameongeza kua mbali na misaada hiyo pia
amewashukuru kwa kuwapatia huduma kwa upande wa mawasiliano ambayo inasaidia
katika upokeaji wa simu wa awali kabla ya kuruka hewani,kwa ajili ya
wasikilizaji ambao wamekua wakitumia vibaya muda wa hewani.
Aidha kaimu mkurugenzi amewataka watangazaji wa radio ulanga kuvitunza
vifaa hivyo katika hali nzuri ili viweze kutumika katika kuboresha vipindi
katika maeneo mbalimbali.
f/mtemangani
ulanga
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Shughuli
za uchomaji mkaa zinaadhiri kwa kiasi
kikubwa hali ya mazingira wilayani ulanga mkoani morogoro.
Hayo
yamesemwa Afisa Misitu wilayani hapo Gerard Kauki wakati akizungumza redio
ulanga fm juu ya hali halisi ilivyo baada ya misitu kuharibiwa wilayani hapo.
Bw Kauki amesema kuwa uharibifu huo
unatokana na wananchi kutofuata kanuni za uchomaji mkaa na kutofahamu kuwa
uchomaji mkaa unaharibu mazingira hususani misitu inayowazunguka.
Aidha
Afisa Misitu huyo amesema kuwa mikakati yao ni kuwataka wananchi
kujiunga katika vikundi ili kijisajili kwa shughuli hiyo ya uchomaji mkaa na
sio kuchoma kiholela ka wanavyofanya hivi sasa.
Michael
No comments:
Post a Comment