Karibu Dj Dukeswagas blog

Tuesday, April 29, 2014

SINTO FAHAMU YA KUREJEA KWA MAWASILIANO KATI YA ULANGA NA KILOMBERO YA ENDELEA

eneo lililosombwa na maji
  • WANG'AMBO WA NG'MBO

Hali ya mawasiliano kati ya Ulanga na Wilaya ya kilombero imeendelea kuwa tete baada ya maji yanayo tegemewa kupungua katika mto Kilombero kuendelea kuwepo bila dariri za kuanza kupungua hususani katika eneo lililo athirika zaidi na maji hayo ambalo ni Kivukoni.

Katika siku ya jana na leo mvua zimeendelea kunyesha katika wilaya ya ulanga na Mkoani Iringa ambako ndiko kuna vyanzo vingi vya mito midogo inayoingiza maji katika mto Kilombero.Hali ya usafirishaji wa mazao kutoka wilaya ya Ulanga kwenda kilombero(Ifakara) imeendelea kuwa tete na ngumu kutokana na magari ya mizigo kushindwa kuvuka katika Mto kilombero Baada ya hivi karibuni kivuko cha Mto kilombero kusimamishwa hadi hapo Maji yatakapo pungua.

Aidha hapo jana moja ya mkulima katika harakati za kuvusha mazao (Mchele) mtumbwi aliokuwa anasafirishia mazao hayo ulipinduka na kuzamisha jumla ya magunia 7 ya Mchele yaliyo kuwa yakisafirishwa baada ya mwendesha mtubwi kutingwa na dereva waboat ndogo inayovusha abiria katika mto huo.


wasafiri katika mtumbwi
kutokana na kukatika kwa mawasiliano kati ya ulanga na Kilombero baadhi ya bidhaa katika wilaya ya Ulanga zimeanza kupanda ambapo katika mji wa Mwaya mafuta ya Petroli ni shilingi 3000 kwa lita huku katika mji wa mahenge bidhaa hiyo kuonekana kugombaniwa na baadhi ya boda boda na watumiaje wengine,ambapo baadhi ya watu wameonekana wakibeba mafuta na kuweka majumbani kama akiba na kusahau hatari inayo weza kujitokeza.

Hadi leo jioni hali imeendelea kuwa tete katika mto kilombero, kufungwa kwa kivuko kunakuja baada ya kivuko hicho kusombwa mara kadhaa na maji hali iliyofanya uongozi kusitisha huduma hiyo kutokana na kuogopa kujirudia kwa tukio la miaka ya nyuma ambapo kivuko cha mwanzo kilizama na kusababisha vifo.
Mabaki ya kivuko kilicho zama miaka ya 2002/03



Monday, April 28, 2014

BAADHI YA HABARI KATIKA TAARIFA YA HABARI YA ULANGA FM USIKU HUU



                                

Halmashuri ya wilaya ya ulanga mkoani morogoro wametoa shukrani kwa shirika la utangazaji lisilo la kiserikali la UINGEREZA  BBC MEDIA ACTION kwa kuwapatia msaada wa vifaa ikiwemo lapto mbili pamoja na maranzi kwa ajili ya kurekodia vipindi vya Radio ulanga kwa ubora.

Hayo yamebainishwa hii leo na kaimu mkurugenzi wa halmashauri bwana Benedict Mabula kwenye ukumbi wa paulin katika siku ya Radio Open Day.

Hata hivyo bwana Mabula ameongeza kua mbali na misaada hiyo pia amewashukuru kwa kuwapatia huduma kwa upande wa mawasiliano ambayo inasaidia katika upokeaji wa simu wa awali kabla ya kuruka hewani,kwa ajili ya wasikilizaji ambao wamekua wakitumia vibaya muda wa hewani.

Aidha kaimu mkurugenzi amewataka watangazaji wa radio ulanga kuvitunza vifaa hivyo katika hali nzuri ili viweze kutumika katika kuboresha vipindi katika maeneo mbalimbali.
f/mtemangani                                                                          ulanga
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx




Shughuli za uchomaji  mkaa zinaadhiri kwa kiasi kikubwa hali ya mazingira wilayani ulanga mkoani morogoro.

Hayo yamesemwa Afisa Misitu wilayani  hapo Gerard Kauki wakati akizungumza redio ulanga fm juu ya hali halisi ilivyo baada ya misitu kuharibiwa wilayani hapo.

Bw Kauki amesema kuwa uharibifu huo unatokana na wananchi kutofuata kanuni za uchomaji mkaa na kutofahamu kuwa uchomaji mkaa unaharibu mazingira hususani misitu inayowazunguka.

Aidha Afisa Misitu huyo amesema kuwa  mikakati yao ni kuwataka wananchi kujiunga katika vikundi ili kijisajili kwa shughuli hiyo ya uchomaji mkaa na sio kuchoma kiholela ka wanavyofanya hivi sasa.

Michael

 

Sunday, April 27, 2014

HALI TETE YA KIVUKO,

Kivuko cha simamishwa kufanyakazi hadi maji yatakapo pungua
Moja ya mchina anaye husika na michoro katika ujenzi wa mto kilombero ajinyonga


Mkuu wa wilaya ya Ulanga Mh, Fransisi Miti leo  amesitisha huduma ya kivuko kati ya ulanga na kilombero kwa kutumia pantoni ya kivuko MV. KILOMBERO hadi hapo maji yatakapo pungua kutokana na kivuko hicho kuzidiwa na nguvu ya maji.

Amewaomba wananchi wa wilaya zote mbili kuto kusafiri kwa muda kwa safari zisizo za lazima   hadi hapo maji yatakapo pungua huku kwa wale wanao lazimika kusafiri sasa kutumia boti ndogo zilizopo na kuacha kutumia mitumbwi ambayo si salama.

Wakati huo huo maji hapo juzi jioni yalikata mawasiliano ya barabara kati ya Ulanga na kilombero kwa kuzoa moja ya kalavati upande wa Ifakara ambapo moja ya gari lilisombwa na maji huku nayo pantoni ilisitisha huduma kwamuda baada ya kusombwa na maji na kupelekwa  upande wa bondeni.

Mitumbwi na boti ndogo zilionekana zikivusha watu hapojuzi huku nauli katika boti na mtumbwi wa kawaida kwa mtu mmoja ikipanda kutoka shilingi 200 ya kawaida hadi 1000 kwa mtu mmoja huku pikipiki zikisafirishwa kwa kati ya shilingi 3000 hadi 8000.

baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi hapo juzi katika eneo hilo la kivukoni wamesema hali mbaya ya usafiri inayojitokeza sasa nikutokana na uzembe wa kutoyatengeneza makalavati hayo katika msimu wa kiangazi huku mamlaka inayohusika na utengenezaji wa barabara katika eneo hilo ikiendelea kukwangua tuta la barabara hiyo lililo wekwa na campuni ya BENACO miaka  hiyo, hali iliyopelekea tutahilo kuwa dhaifu.

Wakati hayo yakiendelea leo imeripotiwa moja ya mchina amejinyonga,
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana zinadai mchina huyo aliyekuwa anahusika na michoro ya ujengaji wa daraja amejinyonga kutokana na upweke uliokuwa unamsibu.

baadhi ya watu wakaribu na vibarua wa ujenzi wa daraja la mto kilombero ambalo bado halija anza kujengwa hadi sasa licha ya kutakiwa kukamilika mwakani wamesema yawezekana mchina huyo amejinyonga kutokana na hali mbaya iliyojitokeza kutokana na kuzama kwa makaravati ambayowalikuwa wamekwisha jenga.

mvua za mwaka huu katika wilaya ya kilombero na Ulanga zinadaiwa kuwa ni kubwa kuwahi kutokea ambapo miundombinu ya barabara iomehalibiwa vibaya.

MATUKIO MBALI MBALI KATIKA PICHA.

Barabara kutoka lupiro kwenda mahenge eneo la Fimbo

Mto Kilombero

Muendesha Mtumbwi Kazini

Moja ya usafiri unaotumika

Moja ya karavati yaliyojengwa na wachina

Karavati jipya

Eneo la barabara Kivukoni upande wa Ifakara

Kalavati likiwa limezamishwa na maji


Kalavati likiwa limemeguka upande

Foleni ya Magari Kabla ya kufikiakivukoni

Katapila likiwa limewekwa katikati ya barabara kuzuia njia watu wasipite kutoa nafasi ujenzi uendelee.

hatariii


kivukoni- hali halisi

eneo  liliosombwa na maji na kuvunja mawasiliano yaUlanga na Kilombero