HISTORIA YA MUUNGANO, JE TWAJIFUNZA NINI
Tanzania ni nchi iliyoko Afrika ya Mashariki. Imepakana na Uganda na Kenya upande wa Kaskazini, Bahari Hindi upande wa mashariki, Msumbiji, Malawi na Zambia upande wa kusini, Kongo, Burundi na Rwanda upande wa magharibi.
Eneo lina kilometa mraba 945,203 (nchi ya 31 duniani); maji ya ndani yanachukua asilimia 6.2.
Idadi ya watu inakadiriwa (mwaka 2010) kuwa 43,188,000 (nchi ya 30 duniani) kutoka 34,443,603 waliohesabiwa katika sensa ya mwaka 2002.
Msongamano ni wa watu 46.3 kwa km2 (nchi ya 124 duniani).
Tanzania ni nchi kubwa zaidi kati ya wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Tanzania ni moja kati ya nchi maskini duniani ambazo zimefanikiwa kufutiwa madeni katika mpango wa kusamehe madeni wa Kundi la Nchi Nane.
Mji mkuu ni Dodoma, lakini makao makuu ya serikali ni bado Dar es Salaam, jiji kubwa zaidi, lenye watu zaidi ya milioni tatu. Majiji mengine ni kama vile Mwanza, Mbeya, Arusha, Tabora na Tanga
Jina "Tanzania" limeundwa
kutokana na majina ya TANganyika na ZANzibar
(pamoja na athira ya jina la kale la "Azania").
Nchi hizo mbili zilikuwa zote chini
ya utawala wa Uingereza
hadi kupata uhuru lakini hazikuwa makoloni ya kawaida.
Zanzibar ilikuwa na hali ya nchi lindwa
kutokana na mikataba kati ya masultani wa Zanzibar na Ufalme wa Muungano (Uingereza).
Tanganyika iliwahi kuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia halafu
ikawa chini ya Uingereza kama eneo la kudhaminiwa kutokana na azimio la Shirikisho la Mataifa iliyoweka Tanganyika
katika ngazi "B" ya maeneo ya kudhaminiwa.
Tanganyika na Zanzibar zilikuwa nchi
mbili tofauti hadi 1964,
zilipoungana na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hapo kiongozi wa
Tanganyika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
alipata kuwa Rais wa
kwanza na kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar Abedi Amani Karume akawa Makamu wa Kwanza wa Rais.
Tanzania, chini ya Rais wa awamu ya
pili Ali Hassan Mwinyi iliruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania na
kuanza mpango wa kurekebisha uchumi kuendana na masharti ya Benki
ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani.
Rais wa awamu ya tatu, Benjamin
Mkapa aliendeleza mfumo wa uchumi wa soko huria ambapo mashirika ya umma
yanabinafsishwa.
Tarehe 21 Desemba
2005 Jakaya
Kikwete ameapishwa kuwa Rais wa nne wa taifa.
Muungano
kati ya Tanganyika na Zanzibar
Tangu muungano wa Tanganyika na
Zanzibar mwaka 1964 Tanzania imefuata miundo ifuatayo:
- Nchi inatawaliwa na serikali ya muungano ikitekeleza sheria zinazotolewa na bunge la Tanzania.
- Tanganyika au Tanzania bara haina serikali wala bunge la pekee.
- Zanzibar (Unguja na Pemba) ina serikali na bunge lake vinavyoratibu mambo yasiyo ya muungano.
Mambo yafuatayo yalikubalika kuwa
shughuli za muungano:
- Mambo ya nje
- Jeshi
- Polisi
- Mamlaka ya dharura
- Uraia
- Uhamiaji
- Biashara ya nje
- Utumishi wa umma
- Kodi ya mapato, orodha
- Bandari, Usafiri wa anga, Posta na Simu
Demografia
Watu wa Tanzania hawaenei sawasawa.
Katika maeneo makavu sana, kunaishi mtu mmoja tu kwenye kilomita moja ya mraba
(1/km²), lakini sehemu zenye rutuba za bara, kuna watu 51 kwa kila
kilomita ya mraba. Hatimaye huku Unguja kuna watu 134 kwa kilomita ya mraba.
Zaidi ya asilimia themanini huishi
vijijini.
Kuna makabila zaidi ya 120. Makabila yenye watu
zaidi ya milioni moja ni Wasukuma, Wanyamwezi, Wachaga, Waha, Wagogo, Wahaya na Wamakonde.
Idadi kubwa sana ya Watanzania ni
jamii ya Wabantu.
Nje ya hao, kuna Waniloti, kwa mfano Wamasai na Wajaluo ambao
wengi wao zaidi wanaishi Kenya. Kundi lingine ni makabila ya Wakushi wanaoishi kaskazini mwa
Tanzania; hao ni makabila ya Wairaqw, Wafiome na Wasi. Kuna vikundi viwili vya Wakhoisan wanaofanana na makabila ya Botswana na Namibia; majina
yao ni Wasandawe
na Waburunge.
Hatimaye kuna Wahadzabe wachache ambao utafiti wa DNA
umeonyesha hivi karibuni wana uhusiano wa asili na Watwa wa nchi za Afrika
ya Kati.
Lugha
Nchini Tanzania kuna lugha za kikabila zaidi ya
mia moja na ishirini. Hakuna lugha rasmi kisheria, lakini Kiswahili
ndiyo lugha ya taifa.
Ingawa kila kabila lina lugha yake,
lugha ya taifa ya Tanzania ni Kiswahili ambacho ni mojawapo kati ya lugha za Kibantu. Hali hii
imesaidia sana kukubaliwa kwa Kiswahili nchini kwa sababu idadi kubwa ya
Watanzania ni wasemaji wa lugha za Kibantu.
Kiswahili kinatumika kama lugha
baina ya watu wa makabila mbalimbali na kwa mambo ya rasmi; kwa hiyo ni lugha
rasmi ya dhati. Baada ya uhuru, Kiingereza
(iliyokuwa lugha ya kikoloni kabla ya uhuru) iliendelea kutumika kwa mambo kadhaa rasmi na kwa elimu kuanzia sekondari, na kwa hiyo ilichukuliwa
kama lugha rasmi ya dhati pamoja na Kiswahili. Lakini utumizi wa rasmi wa
Kiingereza imepungua katika milongo iliyopita, na sasa utumizi huu karibu
umekwisha. Kwa hiyo siku hizi ni kawaida zaidi kuchukulia Kiswahili kama lugha
rasmi ya dhati pekee.
Dini
Makala kuu ya: Dini nchini Tanzania
Nchi haina dini rasmi na katiba ya Tanzania
inatangaza uhuru wa dini kwa wote. Mara nyingi idadi ya wafuasi
wa dini hutajwa kuwa
theluthi moja Waislamu,
theluthi moja Wakristo
na theluthi moja wafuasi wa dini za jadi. Lakini tangu uhuru swali la dini
ya wananchi halijaulizwa tena katika sensa, kwa hiyo
kadirio la theluthi-theluthi halina msingi halisi bali ni zaidi azimio la
kisiasa.
Waislamu hudai mara nyingi ya kwamba
wenyewe ni sehemu kubwa ya Watanzania, angalau zaidi ya nusu. Kamusi ya
"World Christian Encyclopedia" (2002) yataja Wakristo kuwa 52%,
Waislamu kuwa 32% na wafuasi wa dini za jadi kuwa 14%.
Kwenye visiwa vya Zanzibar idadi
ya Waislamu huaminiwa kuwa takriban 95%.
Usafiri
(habari za undani zaidi katika
makala ya Usafiri wa Tanzania)
Usafiri nchini Tanzania ni hasa kwa
njia ya barabara. Mengine ni reli na ndege. Kwenye maziwa makubwa na pwani la
Bahari Hindi kuna pia usafiri kwa meli.
Hadi sasa idadi ya barabara za lami
si kubwa. Kuna hasa njia nzuri kati ya Dar es
Salaam, Mbeya
katika kusini-madharibi, Dodoma katika kitovu cha nchi, Arusha / Tanga katika
kaskazini-mashariki. Kusini-Mashariki na Magharibi ya nchi kwa jumla haina
barabara nzuri na mawasiliano ni magumu.
Shirika mbili za reli zahudumia
Tanzania ni TRC (Shirika ya Reli Tanzania
- Tanzania Railways Corporation) na TAZARA
(Tanzania-Zambia Railways Corporation). TRC imetawala reli ya kati kuanzia Dar
es Salaam hadi Kigoma
halafu reli ya Tanga kati ya Tanga na Arusha. Tazara imeunganisha Dar es Salaam
na kusini ya nchi hadi Zambia. Zote hazikutunzwa vizuri na usafiri unakumbwa na
huduma mbaya pamoja na ajali.
Huduma kwa ndege zatumia hasa nyanja
za ndege 11 penye barabara ya lami kwa ajili ya ndege hasa Julius Nyerere/Dar es
Salaam, Kilimanjaro /Arusha-Moshi
na Zanzibar-Kisauni.
Utamaduni
na sanaa
Bombwe la Kimakonde: Tembo
Kati ya wasanii wa Tanzania ni hasa
wajume wa ubao na wachoraji waliojulikana kimataifa.
Uchongaji wa mabombwe ya Kimakonde
yamesifiwa tangu mwanzo wa karne ya 20. Wamakonde wengi wamehamia Daressalaam au
Arusha wanapohudumia soko la watalii na soko la nje.
Tangu miaka
ya 1970 uchoraji
wa "tingatinga" umejulikana:
ulipata jina hilo kutoka kwa Edward
Tingatinga naye mtu wa Umakonde.
Utamaduni wa
Watanzania ni pamoja na utaraab. Muziki ana nyimbo za kitaraab ndizo muhimu sana kwa nchi
nzima, hasa visiwani na pwani. Pia kuna miziki ya Kinyarwanda,
dansi kama intore n.k.
Urithi
wa Dunia
Mahali pafuatapo katika Tanzania
pamepokewa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi
wa Dunia".
(mwaka wa kukubaliwa - jina la
mahali)
- 1979 – Hifadhi ya Taifa Ngorongoro
- 1981 – Hifadhi ya Taifa la Serengeti
- 1981 – Maghofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara
- 1982 – Hifadhi ya Taifa Selous
- 1987 – Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro
- 2000 – Mji Mkongwe wa Jiji la Zanzibar / Unguja
- 2006 - Michoro ya Kondoa