Kutokuelewana
kwa Mbunge wa Mbeya MH. Joseph Mbilinyi aka SUGU na mkurugenzi wa clouds fm ya
jijini Dar,LUGE hatimaye siku ya
jumatatu ya wiki hii , kumekwisha baada ya wawili hao kukutana na kutangaza
kubalizika kwa ugomvi huo.
Akizungumza katika
mkutano huo uliowahusisha waandishi wa habari mbilinyi aka SUGU amesema kwa
sasa mtafaruku huo umekwisha na kilichobaki ni kufanyakazi kwa kushirikiana
ilikupandisha mziki wa kitanzania na kusimamia haki za wasanii.
Haya ndio aliyoyasema sugu baada ya kumaliza kutoa taarifa ya kupata.
KWANZA
POLENI NA SAMAHANINI KWA HALI YA SINTOFAHAMU ILIYOTOKEA LEO KUTOKANA NA
TAARIFA ZA GHAFLA ZA USULUHISHI KATI YETU NA RUGE/CLOUDS FM,NI KUTOKANA
NA UNYETI WA ISSUE YENYEWE ILIBIDI TUFANYE HIVYO KWA NIA NJEMA
KABISA...KWANZA NAOMBA TUJIPONGEZE KWA KUWA TUKIO LA LEO NI USHINDI KWA
VINEGA KWA MAANA KWAMBA MADAI YETU YOTE YA MSINGI NDIO YALIKUWA MSINGI
WA MAJADILIANO NA RUGE AMEKUBALI KUYATEKELEZA YOTE...
KUANZIA
SUALA LA STUDIO YA RAIS KURUDISHWA KWA BASATA ILI IWE YA WASANII
WOTE,PIA T.F.U IJIKABIDHI KWA CHAMA HALALI CHA WASANII YAANI T.U.M.A
KAMA AMBAVYO TULIKUWA TUNADAI NA MPAKA ISSUE ZA WASANII KUNYANYASWA NA
KUBANIWA NA PIA SUALA LA MALIPO HAFIFU VYOTE VIMEJADILIWA NA KUKUBALIWA
KWA UTEKELEZAJI...HAIKUWA KAZI RAHISI,KWANZA ILIANZA KWA WAO KUMPIGIA
MWENYEKITI WANGU MBOWE KUTAKA TUKAE CHINI,AMBAPO KAMANDA MBOWE
ALINISHAURI TUKAE NAO CHINI KAMA KWELI WANA NIA YA KUYAMALIZA...BAADAYE
WAKAMPIGIA MR SHIGONGO AMBAYE NI WAZI KUWA NI KATI YA WATU WANGU WA
KARIBU NAYE BAADA YA KUONGEA NA MR. KUSAGA TU ALINIPIGIA NA KUNISHAURI
HIVYO HIVYO...
NA
KAMA HAIKUTOSHA WAKALIFIKISHA HILI SUALA KWENYE KAMATI YA BUNGE AMBAYO
ILINITAKA NIIPE MAELEZO YA KIINI CHA MGOGORO NA NIKAFANYA HIVYO AMBAPO
PIA BAADA YA KUNIELEWA WAKASHAURI NIKAE NAO CHINI...NA HATIMAYE SUALA
HILI LIKAISHIA MIKONONI MWA WAZIRI NCHIMBI PAMOJA NA MHE. TUNDU
LISSU(MP) KUWA WAPATANISHI WETU...WAZIRI NCHIMBI AKAANZA KWA KUMUITA
RUGE DODOMA NA ALIKUJA TUKAKAA KWA HATUA YA KWANZA NA HATIMAYE LEO
TUKAKAA TENA MAKAO MAKUU YA WIZARA YA UTAMADUNI CHINI YA DR NCHIMBI NA
MHE TUNDU LISSU NA HATIMAYE TUKAFIKIA HATUA HII YA LEO...VITA YETU
ILIKUWA NA HOJA HATUKUWA TUNAPIGANA TU KWA CHUKI BINAFSI KAMA BAADHI YA
WATU WALIVYOKUWA WANAJARIBU KUIWEKA,KWAHIYO KAMA HOJA ZETU ZIMEELEWEKA
KWA SASA TUNATAKIWA KUSHUKURU NA KUFURAHIA...LAKINI NAOMBA
NIWAHAKIKISHIE MISIMAMO IKO PALE PALE NA NIMEWAWEKA WAZI KUWA ANTI-VIRUS
ITAENDELEA KUWEPO ILI KUENDELEA KU-SCAN VIRUS WENGINE KAMA MAMENEJA
MASOKO NA WENGINE WATAKAOJITOKEZA KWANI NCHI INAPOSHINDA VITA AU HATA
KUFIKIA TU MAKUBALIANO YA AMANI NA NCHI ADUI YAKE HAINA MAANA NCHI HIYO
INAVUNJA JESHI LAKE...
ASANTENI SANA...
ASANTENI SANA...
No comments:
Post a Comment