Karibu Dj Dukeswagas blog

Tuesday, February 21, 2012

SUGU NA LUGE WATANGAZA KUMALIZA BIFU



Kutokuelewana kwa Mbunge wa Mbeya MH. Joseph Mbilinyi aka SUGU na mkurugenzi wa clouds fm ya jijini Dar,LUGE  hatimaye siku ya jumatatu ya wiki hii , kumekwisha baada ya wawili hao kukutana na kutangaza kubalizika kwa ugomvi huo.
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakipeana mikono leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili.
Akizungumza katika mkutano huo uliowahusisha waandishi wa habari mbilinyi aka SUGU amesema kwa sasa mtafaruku huo umekwisha na kilichobaki ni kufanyakazi kwa kushirikiana ilikupandisha mziki wa kitanzania na kusimamia haki za wasanii.

Haya ndio aliyoyasema sugu baada ya kumaliza kutoa taarifa ya kupata.

KWANZA POLENI NA SAMAHANINI KWA HALI YA SINTOFAHAMU ILIYOTOKEA LEO KUTOKANA NA TAARIFA ZA GHAFLA ZA USULUHISHI KATI YETU NA RUGE/CLOUDS FM,NI KUTOKANA NA UNYETI WA ISSUE YENYEWE ILIBIDI TUFANYE HIVYO KWA NIA NJEMA KABISA...KWANZA NAOMBA TUJIPONGEZE KWA KUWA TUKIO LA LEO NI USHINDI KWA VINEGA KWA MAANA KWAMBA MADAI YETU YOTE YA MSINGI NDIO YALIKUWA MSINGI WA MAJADILIANO NA RUGE AMEKUBALI KUYATEKELEZA YOTE...


KUANZIA SUALA LA STUDIO YA RAIS KURUDISHWA KWA BASATA ILI IWE YA WASANII WOTE,PIA T.F.U IJIKABIDHI KWA CHAMA HALALI CHA WASANII YAANI T.U.M.A KAMA AMBAVYO TULIKUWA TUNADAI NA MPAKA ISSUE ZA WASANII KUNYANYASWA NA KUBANIWA NA PIA SUALA LA MALIPO HAFIFU VYOTE VIMEJADILIWA NA KUKUBALIWA KWA UTEKELEZAJI...HAIKUWA KAZI RAHISI,KWANZA ILIANZA KWA WAO KUMPIGIA MWENYEKITI WANGU MBOWE KUTAKA TUKAE CHINI,AMBAPO KAMANDA MBOWE ALINISHAURI TUKAE NAO CHINI KAMA KWELI WANA NIA YA KUYAMALIZA...BAADAYE WAKAMPIGIA MR SHIGONGO AMBAYE NI WAZI KUWA NI KATI YA WATU WANGU WA KARIBU NAYE BAADA YA KUONGEA NA MR. KUSAGA TU ALINIPIGIA NA KUNISHAURI HIVYO HIVYO...

NA KAMA HAIKUTOSHA WAKALIFIKISHA HILI SUALA KWENYE KAMATI YA BUNGE AMBAYO ILINITAKA NIIPE MAELEZO YA KIINI CHA MGOGORO NA NIKAFANYA HIVYO AMBAPO PIA BAADA YA KUNIELEWA WAKASHAURI NIKAE NAO CHINI...NA HATIMAYE SUALA HILI LIKAISHIA MIKONONI MWA WAZIRI NCHIMBI PAMOJA NA MHE. TUNDU LISSU(MP) KUWA WAPATANISHI WETU...WAZIRI NCHIMBI AKAANZA KWA KUMUITA RUGE DODOMA NA ALIKUJA TUKAKAA KWA HATUA YA KWANZA NA HATIMAYE LEO TUKAKAA TENA MAKAO MAKUU YA WIZARA YA UTAMADUNI CHINI YA DR NCHIMBI NA MHE TUNDU LISSU NA HATIMAYE TUKAFIKIA HATUA HII YA LEO...VITA YETU ILIKUWA NA HOJA HATUKUWA TUNAPIGANA TU KWA CHUKI BINAFSI KAMA BAADHI YA WATU WALIVYOKUWA WANAJARIBU KUIWEKA,KWAHIYO KAMA HOJA ZETU ZIMEELEWEKA KWA SASA TUNATAKIWA KUSHUKURU NA KUFURAHIA...LAKINI NAOMBA NIWAHAKIKISHIE MISIMAMO IKO PALE PALE NA NIMEWAWEKA WAZI KUWA ANTI-VIRUS ITAENDELEA KUWEPO ILI KUENDELEA KU-SCAN VIRUS WENGINE KAMA MAMENEJA MASOKO NA WENGINE WATAKAOJITOKEZA KWANI NCHI INAPOSHINDA VITA AU HATA KUFIKIA TU MAKUBALIANO YA AMANI NA NCHI ADUI YAKE HAINA MAANA NCHI HIYO INAVUNJA JESHI LAKE...

ASANTENI SANA...

Saturday, February 18, 2012

THE BEAT POWER TOP 20 (BPT20)


 ULANGA FM
 (BPT20)
Nikipindi cha burudani ambacho huruka hewani kilasiku za juma pili kikichambua na kuupangilia muziki wa kizazi kipya alimaarufu kama bongo fleva kuanzia nafasi ya 20 hadi ya 1, Dj DUKE ndio dereva wa kipindi hiki kuanzia 10 kamili za jioni hadi 1:00 kamili za jioni


Dj duke
Furahia muziki wa kizazi kipya kila jumapili na dj duke Halaaaaaa. cheki chini hiyo ni chati mpya ya top 20 ulanga fm enjoy people.

 NEW  THE BEAT POWER TOP 20
                        (BPT 20)
No 20         Fid q farid kubanda… ielewe mitaa
No 19         Izo busness fet dully….barua pro fish club
No 18         lakuchumpa la kumparama…. Godzilar fet jot
N0 17         bellinine …. Amerudi
No 16         magube gube ….. baranaba
No 15         Alikiba fet lad j dee…. Single boy
No 14         mbayu wayu….. mallow
No 13         kizungu zungu…. Abdukiba
No 12         richimavocal…. Silali
No 11         bagdadi fet climaxbibo…. Oh mama
N0 10         nivute kwako … Dyna fet barnaba
No 9           maneno maneno…. Quen Doreen
No 8           stamina fet rich mavocal…. Kabwela
No 7           youg dee fet katokololo…. Dada huyo
No 6           20%..... si mfano
No 5           AT…. bao la kete
NO 4          diamond plat nam…. Nimpende nani.
No 3           kichwa kinauma….. tmk
No 2           aslay ….. naenda kusema
Bonas         bwana shamba… mchovu
No 1           ukweli wa moyo…. Ney wamitego fet matonya                         
                  

NI MIAKA 27 YA KUISHI KWANGU

l
Kila febr 18.02 Dj DUKE husherekea siku yake ya kuzaliwa, nam leo naungana nawengine wengi katika kusherekea siku yangu ya kuzaliwa hii ni siku yangu ya kuzaliwa ya 27 toka nifike kwa dunia.Shukrani zimuendee mama mzazi kwa kunilea hadi kufikia hapa nilipo. mungu anitangulie kwa mengi. halaaa all ma fans.

Mengi hutokea katika maisha yetu baadhi yetu hukata tamaa na kuamua kuyakatisha maisha yao lakini kwakufanyaa hivyo twamchukiza mungu yatupasa kupambana na maisha na kuhakikisha daima tuna yashinda, misingi bora iandaliwayo na wazazi wetu huwa nguzo bora ya maisha ya maanikio kwetu baadae. mungu aniongoze na mungu atuongoze vijana wa taifa hili katika kupambana na maisha haya magumu ya sasa. Ameni.
DJ DUKE & DEO 

Wednesday, February 8, 2012

ISHU YA TIMBULO KUKOPI NYIMBO KUTOKA KWA X-MALEYA

Msanii kutoka bongo anayejulikana kwa jina la Timbulo ambaye alitoka na wimbo wake wa kwanza unaojulikana kwa jina la Domo Langu na wa pili Waleo wa Kesho na kuteka wabongo wengi sana, sasa imegundulika kuwa jamaa amewacopy wasanii X  Maleya kutoka Cameroon.
Bado sijajua je mwenye makosa ni producer wake aliyemtengenezea biti anajulikana kama Lil Gheto au ni yeye Timbulo ndio aliyempa melody producer?
 

Tuesday, February 7, 2012

Geofrey Liduke ndio jina langu nililopewa na mama mzazi Liliani Barnabas mimi ni mzaliwa wa Iringa -Njombe, asili ya watu kutoka kaskazini, watu wengi wananifahamu kwa jina la Dj duke. kutokana na kazi yangu ya utangazaji. karibu katika blog hii. hapa utapata habari mbalimbali na mengineo mengi karibu.